Dhana ya neno “Tafsiri” imeelezwa na watalamu mbalimbali na
kwa nyakati tofauti tofauti kama ifuatavyo:
Kwa mujibu wa (1965:20). Tafsiri ni ni kuchukua mawazo yaliyo
katika maandishi kutoka lugha moja (lugha chanzi) na kuweka badala yake mawazo
yanayolingana na hayokutoka lugha nyingine (lugha lengwa).
TUKI, (2002). Tafsiri ni kutoa mawazo katika lugha moja
kwenda lugha nyingine bila kubadilisha maana.
Mwansoko na wenzake, (2006). Wanafasiri tafsiri kuwa ni zoezi
la la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja kwenda lugha
nyingine.
Mshindo, (2010) anasema, kufasiri ni kufafanua maana ya matini
moja na kutayarisha baadae matini nyingine inayowiana nayo ambayo inawakilisha
ujumbe uleule uliokuwa katika matika matini ya awali kwa kutoka lugha nyingine.
Newmark (1992), Tafsiri ni jaribio la kuwasilisha ujumbe
uleule ulioandikwa katika lugha moja kwa lugha nyingine.
AS-Safi akimnukuu Dubois (1982) anaeleza kuwa tafsiri ni
uelezaji wa mawazo katika nyingine (lugha lengwa) wa kilichoelezwa katika lugha
nyingine (lugha chanzi).
Larson (1984) anaeleza
kuwa, Tafsiri inahusisha uhawilishaji wa maana iliyoko katika maandishi katika
lugha chanzi kwenda lugha lengwa.
Katika maana zote hizi, tunaona kuwa ndani ya fasili ya
tafsiri kuna mambo matatu mhimu ambayo ni:
·
Ujumbe
au mawazo yanayotakiwa kutafsiriwa sharti yawe katika maandishi.
·
Mawazo
au ujumbe katika lugha chanzi na lugha lengwa sharti yalingane.
·
Tafsiri
inaweza kuwa kutoa maana ya maneno au mawazo.
Hivyo, tafsiri ni zoezi la uhawilishaji wa mawazo, ujumbe au
taarifa iliyopo katika maandishi kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa bila
kupoteza maana ya msingi na mtindo uliotumika katika matini chanzi.
Wanjala (2011) anaeleza kuwa, historia ni taarifa, maelezo na
ucahambuzi wa matukio, watu na nyakati teule zinazoathiri maisha ya wanajamii
husika, sasa na siku za usoni. Ujuzi wa historia hutuwezesha kuthibiti na
kuthamini misingi na maendeleo ya taaluma zetu. Ufafanuzi wa historia ya
tafsiri kidunia, huelezewa kupitia vipindi bainifu vitano vya tajiriba ya
binadamu kwa kuegemea maendeleo na utamaduni.vipindi hivyo ni:
·
Enzi
za kale (old age),
·
Enzi
za giza ( the dark age),
·
Enzi za ufufuko (Renaissance period),
·
Enzi
za kati (middle age),
·
Enzi
za sasa (late age).
Historia ya tafsiri nchini Tanzania haina mda mrefu sana
kwani inaanzia mnamo karne ya 19 ambayo tunaweza kugawa historian a maendeleo
katika vipindi vitatu ambavyo ni: Kabla ya utawala wa kikoloni, Wakati wa
utawala wa kikoloni na baada ya uhuru.
Kabla ya utawala wa kikoloni. Kaika kipindi hiki, Wamisionari
walitafsiri vitabu mbalimbali vya kikristo ikiwemo Biblia takatifu kutoka lugha
ya kiingereza kwenda Kiswahili na lugha nyingine za makabila kwa lengo la
kueneza dini na ustaarabu wa kikristo kwa waafrika.
Wakati wa utawala wa kikoloni. Hiki ni kipindi
kuanzia miaka ya 1800. Katika kipindi hiki wakoloni hasa waingereza walitafsiri
maandiko mbalimbali ya kitaaluma na fasihi ya ulaya kwa lugha ya Kiswahili.
mfano, Fasihi zilizotafsiriwa ni tamthiliya ya Mzimu wa Watu
wa Kaleiliyotafsiriwa na Mohamed S. Abdalla (1960) kutoka lugha ya kiingereza (Shrine
of The Ancestors)
Baada ya uhuru ambayo ni kuanzia
wakati 1961. Katika kipindi hiki wapo wataalamu waliofanya juhudi za kutafsiri
vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili mfano mzuri ni Mwalimu Julius K.
nyerere ambaye alitafsiri vitabu viwili vya mwandishi mashuhuri wa tamthiliya
wa huko Uingereza William Shakespeare ambavyo ni tamthiliya ya Julias kaizari
(Julius Caesar) (1963) na tamthiliya ya Mapebari wa Venis (The Mechant of
Venis) (1969). Kazi nyingine zilizotafsiriwa baada ya ukoloni ni pamoja na kitabu cha ushairi cha Wimbo wa
Lawinoiliyotafsiriwa na Paul Sozigwa (1975) kutoka lugha ya kiingereza (Song of
Lawino), riwaya ya Uhuru wa Watumwa iliyotafsiriwa na East African Litertature
Bureau (1967) kutoka lugha ya kiingereza (The freeing of The Slaves in East
Africa). Pia kazi nyingine za fasihi
zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili hapa Tanzania ni pamoja na na Nitaolewa
Nikipenda ambazo kimetafsiwa na Crement M. Kabugi (1982) kutoka lugha ya
kiingereza ( I will merry When I Want).
Kwa sasa maendeleo ya tafsiri
nchini Tanzania yamepiga hatua kubwa
kutokana na kukua kwa sayansi nta teknolojia. Taaluma ya tafsiri kwa
sasa inafundishwa katika elimu ya sekondari na vyuo mbalimbali. Pia, taasisi na
asasi zinazojishughulisha na tafsiri zimeongezeka. Kwa mfano, Baraza la
Kiswahili Zanzibar (BAKIZA), Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni
(TAKILUKI), Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili (TATAKI) na International Language Orientation Services (ILOS). Pia,
wapo wafasiri mbalimbali binafsi wanaofasiri lugha wanaofasiri lugha mbalimbali
kama vile Kiingereza, Kiswahili, Kiarabu, na Kifaransa.
Hivyo, Taaluma ya tafsiri inazidi
kukua hadi karne kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayofungamana
na maendeleo ya taaluma ya lugha na ongezeko la mataifa huru yanayozungumza
lugha tofauti. Kwahyo, tafsiri ni kama nyenzo kuu ya kuunganisha watu wa
mataifa haya na hutumika kama njia kuu ya mawasiliano.
MAREJEO
As-Safi (1997) “Translation theories, strategies”.
Cartford, (1965). A linguistic Theory Translation.
Mshindo B.H, (2010). Kufasiri na Tafsiri. Oxford University
Press. Dar es salaam.
Mwansoko na Wenzake, (2006). Kitangulizi cha Tafsiri,
Nadharia na Mbinu. TUKI. Dar es salaam.
Sofer. M, (2006). The Translator’s Handbook. Schreiber
Publishing Rockville. U.S.A.
Wanjala, S. F. (2011). Misingi ya Ukalimani na Tafsiri. Kwa
shule, vyuo na ndaki. Serengeti
Bookshop. Mwanza.
Comments
Post a Comment