Posts

Showing posts from November, 2017
Dhana ya neno “Tafsiri” imeelezwa na watalamu mbalimbali na kwa nyakati tofauti tofauti kama ifuatavyo: Kwa mujibu wa (1965:20). Tafsiri ni ni kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja (lugha chanzi) na kuweka badala yake mawazo yanayolingana na hayokutoka lugha nyingine (lugha lengwa). TUKI, (2002). Tafsiri ni kutoa mawazo katika lugha moja kwenda lugha nyingine bila kubadilisha maana. Mwansoko na wenzake, (2006). Wanafasiri tafsiri kuwa ni zoezi la la uhawilishaji wa mawazo katika maandishi kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Mshindo, (2010) anasema, kufasiri ni kufafanua maana ya matini moja na kutayarisha baadae matini nyingine inayowiana nayo ambayo inawakilisha ujumbe uleule uliokuwa katika matika matini ya awali kwa kutoka lugha nyingine. Newmark (1992), Tafsiri ni jaribio la kuwasilisha ujumbe uleule ulioandikwa katika lugha moja kwa lugha nyingine. AS-Safi akimnukuu Dubois (1982) anaeleza kuwa tafsiri ni uelezaji wa mawazo katika nyin